Juba yakanusha kuwapokea Wapalestina

WIZARA ya Mambo ya Nje ya Sudan Kusini imekanusha ripoti zinazodai kuwa imefanya mazungumzo na Israel kuhusu kuwapokea Wapalestina kutoka eneo la Gaza lililoathiriwa na vita.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Associated Press (AP) limesema kuwa Israel inazungumza na Sudan Kusini ili kuwapatia makazi Wapalestina kutoka Gaza, lakini serikali nchini humo imedai kuwa taarifa hizo hazina msingi wowote.

Hata hivyo, wizara hiyo imethibitisha kumpokea Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, Sharren Haskel, aliyefanya ziara mjini Juba jana, na kueleza kuwa mazungumzo yao yalilenga kuimarisha ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii