Kabwe yaibuka kidedea mchakato wa kura Jimbo la Kigoma Mjini za maoni
Kiongozi mstaafu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameibuka kidedea katika mchakato wa kura za maoni za kuwania Jimbo la Kigoma Mjini uliofanyika Agosti 12 mwaka huu.
Katika mchakato huo uliofanyika mkoani Kigoma, Zitto ambaye ni mjumbe wa kamati kuu ya ACT Wazalendo, alipata kura 228 dhidi ya 37 alizozipata Nondo ambaye ni mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ya chama hicho. Jumla ya kura zilizopigwa zilikuwa 269 kati ya hizo, nne ziliharibika.
Kwa matokeo hayo, Zitto ambaye ni mbunge wa zamani wa jimbo hilo, anasubiri kupendekezwa kamati kuu ya chama hicho, ili kuchukua fomu za uteuzi zitakazoanza kutolewa kesho Alhamisi Agosti 14,2025 na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC).
Leo Jumatano Agosti 13, mwaka huu vyombo vya habari vilimtafuta Katibu wa Idara ya Oganaizesheni wa ACT Wazalendo, Shaweji Mketo aliyesema kwa sasa yupo ‘busy’ kusimamia chaguzi zingine zinazoendelea katika majimbo mbalimbali.
“Naomba nikupigie baadaye nitakupa matokeo yote, bado tunaendelea kuyachakata hapa,” amesema Mketo ambaye pia ni mtiania wa ubunge wa Kilwa Kaskazini mkoani Lindi.
Kwa mujibu wa Ado, majimbo ya Kivule, Chamazi, Kinondoni jana yalitarajiwa mchakato wa kura za maoni ili kuwapata watiania watakaopitishwa katika kikao cha kamati kuu ya chama hicho kitakachoketi siku chache zijazo.
Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii