Makamanda wa kijeshi jijini Khartoum waahidi kuondoa vikosi vyake nchini humo

Makamanda wa kijeshi jijini Khartoum siku ya Jumapili wameahidi kuondoa vikosi vyao kwenye mji huo na kuahidi  kwamba hawatawaunga mkono wapiganaji wowote watakaosalia baada ya makubaliano ya mwisho yaliyokwisha kukamilika

Ahadi hiyo  ilitolewa wakati wa mkutano wa kamati ya serikali iliopewa jukumu la kumaliza vikundi vya kijeshi kwenye mji huo.

Hatua hii ni sehemu ya juhudi za kuondoa vikundi vya kijeshi na kuruhusu maelfu ya raia waliokimbia makazi kutokana na vita kati ya jeshi na wapiganaji wa RSF kurejeale maisha yao ya kawaida.

Mnamo mwezi Julai 18, kiongozi wa kijeshi Jenerali Abdel Fattah al-Burhan aliunda kamati ya kufuatilia kuondolewa kwa makundi yenye silaha na kuandaa kurejea kwa raia kwenye mji huo.

Hatua hii ya kuyaondoa makundi yaliojihami inatazamwa kuwa muhimu wakati huu serikali ikipanga kurejea mjini Khartoum kutoka katika makao yake ya sasa ya Port Sudan.

Wiki iliopita, Waziri Mkuu kamil Idris alitangaza kuwa taasisi za serikali zitarejea jijini Khartoum mwezi Oktoba mpango uliosambamba na kufunguliwa tena kwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Khartoum.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii