Benjamin Netanyahu" Mpango mpya wa Israel kwa Gaza ndio 'njia bora ya kumaliza vita"

Mpango mpya wa Israel wa kuuteka mji wa Gaza "hauna lengo la kuikalia kwa mabavu Gaza," Benjamin Netanyahu amebainisha siku ya Jumapili, Agosti 10, akiuona kuwa "njia bora ya kumaliza vita" ambavyo vimeendelea kwa miezi 22 katika ardhi ya Palestina. 

"Tumekamilisha sehemu kubwa ya kazi leo. Tuna karibu 70% hadi 75% ya Gaza chini ya udhibiti wa kijeshi wa Israeli," Waziri Mkuu wa Israel almetangaza wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Jerusalem.

"Lakini bado tuna ngome mbili zilizosalia: Mji wa Gaza na kambi" katikati mwa Ukanda wa Gaza. "Hatuna chaguo lingine kumaliza kazi", amesema Waziri mkuu wa Israel. 

"Kulingana na mpango ulioidhinishwa na baraza la usalama la Israel siku ya Ijumaa, jeshi "linajiandaa kuchukua udhibiti wa mji wa Gaza," ambao umeharibiwa kwa kiasi kikubwa kaskazini mwa eneo hilo, "wakati wa kusambaza misaada ya kibinadamu" nje ya maeneo ya mapigano. Mpango huo mpya "hauna lengo la kuikalia Gaza, bali kuondoa watu wanaomiliki kinyume cha sheria huko Gaza," ameongeza.

Wakati huo huo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limefanya mkutano wa dharura huko Gaza siku ya Jumapili, Agosti 10, kufuatia tangazo la mpango wa Israel wa kuudhibiti mji huo. Wakati huo huo hali inaendelea kuwa mbaya zaidi katika Ukanda wa Gaza. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameionya Israel kuhusu "hatari ya kuongezeka kwa mgogoro", na hivyo "kuhatarisha hali ambayo ni mbaya zaidi kwa mamilioni ya Wapalestina." Lawama zimekuwa zikimiminika tangu kutangazwa kwa mpango huo.

Siku ya Jumamosi, Agosti 9, baadhi ya nchi ishirini za Kiarabu na Kiislamu zililaani mpango wa Israel wa kuchukua udhibiti wa Mji wa Gaza, pia zikiuelezea kama hatari ya kuongezeka kwa mgogoro. "Hii ni changamoto isiyo na kifani na uchochezi kwa nia ya kimataifa ya kufikia amani," Mamlaka ya Palestina imebainisha huko Ramallah.

Brazil, kwa upande wake, imetoa wito wa "kuondolewa kikamilifu na mara moja kwa wanajeshi wa Israel" kutoka Gaza na kusisitiza haja ya dharura ya kusitisha mapigano.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii