Marekani yajenga kituo cha wahamiaji Texas

SERIKALI ya Marekani imejenga kituo chake cha kwanza kikubwa cha kuhudumia wahamiaji katika kambi ya jeshi la Fort Bliss, jimboni Texas, karibu na mpaka wa Mexico.

Kwa mujibu wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon), hatua ya awali ni kuwapatia hifadhi wahamiaji 1,000 kuanzia mwezi huu, katika kituo hicho kilichopewa jina la Camp East Montana.

Pentagon imesema kituo hicho kitapatiwa upanuzi katika wiki na miezi ijayo, ili kutoa huduma za malazi na vitanda kwa wahamiaji 5,000, hatua inayolenga kupunguza msongamano kwenye maeneo mengine ya mpakani.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii