Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), mapigano yamerekodiwa tena wikendi hii kati ya kundi la waasi la AFC/M23 na jeshi la Kongo linaloungwa mkono na Wazalendo. Mapigano haya yalifanyika katika maeneo kadhaa kadhaa, katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Kusini, licha ya kusainiwa kwa usitishaji mapigano, huko Doha, kati ya Kinshasa na AFC/M23.
Katika mkoa wa Kivu Kaskazini, mapigano yaliripotiwa siku nzima ya Ijumaa, Agosti 8, katika eneo la Waloa Yungu. Wakazi walilazimika kukimbia makazi yao. Mashirika ya kiraia ya eneo hilo yana wasiwasi kuhusu nia ya kundi hilo la wapiganaji kuuteka mji wa kimkakati wa Pinga. Kundi la M23 limeripotiwa wapiganaji wa ziada na risasi.
Katika mkoa wa Kivu Kusini, wakati huu, kundi lenye silaha limeteka miji mipya baada ya mapigano makali katika eneo la Mulamba, kulingana na vyanzo vya mashirika ya kiraia huko Walungu.
Jeshi la Kongo, kwa upande wake, linasema kuwa hizo ni taarifa za uongo.
Serikali ya mkoa, kwa upande wake, inaonekana kuthibitisha kutekwa kwa miji katika eneo la Mulamba. Didier Kabi, msemaji wa serikali ya Kivu Kusini, ameshtumu kitendo cha AFC/M23 kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano: "Kutokana na uwepo wa wanajeshi waliotumia na maagizo ya jeshi letu kuangalia usitishaji huo wa mapigano, askari wetu wa FARDC-pamoja na wapiganaji wetu kutoka kundi la Wazalendo-wamejiondoa taratibu ili kuepusha umwagaji damu. Baadhi ya miji - Kanyola, Muzinzi, Ciruko na sehemu ya Mulamba imetekwa na waasi hawa."
Pia katika mkoa wa Kivu Kusini, mapigano mengine yameripotiwa katika eneo la Fizi, huko Kipupu na Mikenge, kulingana na vyanzo vya afya na vya ndani.