Putin na Trump kukutana Alaska wiki hii

VIONGOZI wa Umoja wa Ulaya (EU) wamemuomba Rais wa Marekani, Donald Trump, kuhakikisha usalama wao katika mkutano wa kilele na Rais wa Urusi, Vladimir Putin, unaotarajiwa kufanyika wiki hii utakaojadili vita vya Ukraine.

Viongozi hao wameeleza kuwa wanatarajia kikao hicho kiwe na ushawishi wa kumaliza mgogoro wa Ukraine. Mkutano huo unatarajiwa kufanyika Ijumaa, ingawa viongozi wa EU hawajalikwa kushiriki.

Hadi sasa haijafahamika iwapo Ukraine itahudhuria kikao hicho kitakachofanyika Alaska.

Awali, Trump alisema anataka kukutana na Putin ili kubaini kama ana nia ya kweli ya kumaliza vita hivyo, ambavyo sasa vipo katika mwaka wake wa nne.

Kauli ya Trump kwamba Ukraine inapaswa kuyaachia maeneo yake kwa Urusi, huku Urusi pia ikubali kubadilishana maeneo, kauli ambayo iliwashtua washirika wake wa Ulaya.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii