Msanii Chimano aliyekuwa ni miongoni mwa kundi la Muziki la Sauti Sol kutoka Nchini Kenya, amemuomba msanii mwenzake Bien apokee simu zake kwa sababu amekuwa akimtafuta kwa muda sa sa pasipo bila mafanikio yoyote.
Akizungumza katika mahojiano na Mtandao wa “Okay Africa” nchini Uingereza, Chimano ameeleza kuwa moja kati ya watu ambao anatamani kumshirikisha katika kazi zake kwa hivi sasa, ni pamoja na Bien ambaye haelewi ni kwanini “haokoti” simu zake kwa ajili ya mazungumzo ya kazi, ilihali walikuwa pamoja katika kundi hilo la Sauti Sol
“Bien Tafadhari naomba unipigie ndugu yangu. Ninakutafuta sana na simu zangu haupokei, sijui ni kwanini. Naomba unipigie Bien, kumbuka tulikuwa pamoja katika Bendi” alisikika akisema Chimano
Kauli hiyo imezua maswali kadhaa kwa mashabiki wa Kundi hilo ambalo limevunjika hivi karibuni hasa kuhusu ukaribu wao