Mafanikio katika sekta ya madini ni pamoja na kuongezeka kwa uzalishaji wa madini kutoka tani 7.9 mwaka 2020 hadi tani 42.5 mwaka 2025 hivyo jumla ya
madini yaliyopatikana ni tani 50.4.
Hii imechangia kuongezeka kwa fedha za kigeni kutoka Dola za Marekani milioni 44.33 mwaka 2020 hadi milioni 191.15 mwaka 2025.
Mapato ya Halmashauri kutoka Shilingi milioni 745.4 mwaka 2020 hadi Shilingi 3,334,265,389.56 mwaka 2025; vituo vya ununuzi wa madini kutoka 6 mwaka 2020 hadi 12 mwaka 2025; utoaji wa leseni kwa wachimbaji wadogo kutoka 332 mwaka 2020 hadi 1,766 mwaka 2025.
Makusanyo ya maduhuli kutoka Shilingi bilioni 103.4 mwaka 2020/21 hadi Shilingi bilioni 607.04 mwaka 2024/25; na kuanzishwa kwa masoko ya madini katika Wilaya za Kahama na Shinyanga.