Mkuu wa Wilaya ya Songwe Mh. Fadhili Nkurlu na Mwenyekiti wa Baraza la Biashara,Viwanda na kilimo Tanzania Wilaya ya Songwe ameongoza Mkutano wa Baraza la Biashara la Wilaya lililofanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Solomon Itunda.
Katika Mkutano huo ambao ni Jukwaa linalotoa fursa ya ushirikiano baina ya Sekta ya Umma na Sekta binafsi ,na kujadililiana Kwa pamoja katika kuboresha mazingira ya biashara na Uwekezaji Wilayani Songwe DC Nkurlu amewahimiza Wafanyabiashara kuboresha mahusiano na Serikali ili kuchochea Maendeleo ya kiuchumi kupitia ushirikiano ambao ni sehemu ya Utekelezaji wa Dira ya Taifa na Maendeleo na mkakati wa kukuza Uchumi wa ndani ya Wilaya.
Aidha DC Nkurlu amewakumbusha washikiriki wa Mkutano huo kujiandaa kushiriki Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29 ,2025 Kwa amani na utulivu.
"Jiandaeni kushiriki Uchaguzi Mkuu Kwa amani ili mpate Viongozi ambao wataendelea kutetea maslahi ya Wafanyabiashara na Taifa Kwa ujumla"