TAARIFA : Afande Sele Amvalisha Mpenzi wake Pete Ya Uchumba

Msanii Mkungwe wa Muziki wa Bongo Fleva, Selemani Msindi maarufu kama "Afande Sele" hatimaye amemvalisha pete ya Uchumba mwanamke anayesadikika kuwa ni Mpenzi wake.

Kupitia Ukurasa wake wa Instagram, Afande Sele “Mfalme Wa Rhymes” amepost picha mbali mbali za tukio hilo, huku akisema kuwa watu wajiandae kukamilisha jambo lake Mkoani Morogoro Hivi Karibuni

“Mwanzo na mwisho wa maisha ya maanaadamu ni hapahapa Duniani..

Kuzaliwa...

Kuoa/kutolewa...

Kufa/Kifo.....

Kazi ya hayo mambo muhimu matatu,mawili ni yalazima,lakini moja ni la hiyari na hilo moja la hiyari ndio Jambo pekee unaloweza kulipangia muda na ndio Jambo pekee unaloweza kulishuhudia na kufurahia.

Tukutane kwetu Morogoro mapema Desemba kwajili ya kukamilisha Jambo letu” Ameandika Afande Sele

Afande Sele ni Miongoni mwa Wasanii wachache ambao mahusiano yao yamekuwa na Usiri sana.

Kila la Heri Afande Sele


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii