Anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa Kumuweka Mtoto Wake Kwenye Begi La Nguo

Mwanamke mmoja raia wa Australia, anashikiliwa na Jeshi la Polisi nchini humo baada ya kubainika kuwa alimuweka mtoto wake mwenye umri wa miaka miwili ndani ya Begi la nguo.


Kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini New Zealand ambako tukio hilo lilibainika, mwanamke huyo (Mwenye miaka 27) alikamatwa mara moja baada ya Dereva wa Basi la abiria alilokuwa akilitumia kusafiri kuingia nchini humo (New Zealand) kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama.


Akizungumza na vyombo vya habari, Afisa wa Polisi aliyetambulika kwa jina la Simon Harris amesema kuwa walifanikiwa kufika eneo la mpaka wa Kaiwaka na kumkamata mwanamke huyo, huku mtoto wake akikutwa katika hali ya Joto kali, licha ya kutokuonekana kuwa na madhara mengine kimwili, mtuhumiwa alirudishwa nchini Australia ambako ndiyo makazi yake sambamba na binti yake huyo.


Kwa mujibu wa Dereva wa Basi hilo, waligundua kuwa katika Begi hilo kuna kitu kisicho cha kawaida kutokana na begi kutikisika mara kwa mara, na baada ya kulifungua wakabaini kuwa kulikuwa na mtoto mwenye miaka miwili.


Pia, imebainika kuwa mwanamke huyo hakuwa sawa kiakili, hivyo uchunguzi Zaidi wa kiafya unafanyika juu yake na kisha taratibu nyingine za kisheria ziendelee


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii