Kutana Na Kijana Aliyekataa Ofa Ya Dola Bilioni 1 Kutoka kwa Mmiliki Wa Facebook

Kijana mmoja raia wa Australia ambaye ni mtaalamu wa Akili Mnemba (Artificial intelligence- AI), amekataa Ofa ya kiasi cha USD Bilioni 1 kutoka kwa Bosi wa Facebook, Mark Zuckerberg.

Kwa mujibu wa gazeti la Wall Street Journal kutoka nchini Marekani, kijana huyo huyo anayefahamika kwa jina la Andrew Tulloch ambaye ni muhitimu wa Chuo Kikuu cha Sydney, alikataa “Dili” la kumuuzia Zuckerberg mabala yake yote yenye mashine za Akili Mnemba kwa kiasi hicho cha USD Bilioni 1 (USD 1.5) sawa na Tshs Trilioni 2.4 (2,495,954,680,000/=) kwa madai kuwa Ofa hiyo sio sahihi kwake nan i kama kichekesho kiuhalisia.

Tulloch ambaye awali alikuwa ni Mhandisi katika kampuni ya META ambayo inamilikiwa na Mark Zuckerberg na baadaye kuondolewa katika kampuni hizo kwa sababu za kiutendaji, alianzisha Maabara hiyo akishirikiana na Mira Murati ambaye hivi sasa ni Afisa wa juu katika kampuni ya OpenAI.

Kwa Mujibu wa baadhi ya marafiki wa Tulloch ambao walifanya naye kazi kabla ya kuondolewa katika Kampuni ya META, wanathibitisha kuwa kijana huyo ana uwezo mkubwa wa kufikiria na ana kipaji cha hali ya juu kuliko kawaida.

Aidha, Kampuni ya META ilimuomba Tulloch awauzie maabara hiyo iliyosheheni mashine za AI zenye uwezo mkubwa kwa kiasi hicho cha fedha ambacho kitakuwa kikitolewa kwa awamu ndani ya Miaka Sita, lakini kijana huyo ametupilia mbali ombi hilo huku akwashangaza wengi juu ya Maamuzi yake

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii