Aaron Kalikawe na Luhaga Mpina wapitishwa kugombea urais kwa tiketi ya ACT Wazalendo Tanzania bara

Chama cha ACT Wazalendo kimetangaza rasmi majina ya wagombea wa nafasi za Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Urais wa Zanzibar kupitia chama hicho, kufuatia kikao maalum cha Halmashauri Kuu ya Taifa kilichofanyika  Agosti 5 mwaka huu katika ukumbi wa Hakainde Hichilema.

Katika kikao hicho Halmashauri Kuu ya Chama ilijadili na kupitisha mapendekezo ya wagombea watakaowakilisha chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Wagombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majina mawili yamependekezwa kwa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ni Aaron Kalikawe na Luhaga Mpina. 

Wagombea hawa wawili watawasilishwa kwa Mkutano Mkuu wa Taifa wa chama kwa ajili ya kupigiwa kura na mmoja wao atachaguliwa kuwa mgombea rasmi wa urais kupitia ACT Wazalendo.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii