MJI wa kihistoria wa Hiroshima nchini Japan umeadhimisha kumbukumbu ya miaka 80 tangu Marekani ilipoushambulia kwa bomu la atomiki mashambulizi yaliyochangia kumalizika kwa Vita vya Pili vya Dunia.
Shambulio hilo lililotokea Agosti 6, 1945 liliua takribani watu 140,000 na siku tatu baadaye bomu jingine lilirushwa Nagasaki na kuua wengine 70,000.
Wakati wa maadhimisho hayo baadhi ya waathirika wa tukio hilo waliendelea kuelezea masikitiko yao juu ya namna baadhi ya viongozi wa dunia wanavyotetea matumizi ya silaha za nyuklia kama ishara ya nguvu za kijeshi.
Mashambulizi hayo yalikuwa sehemu ya mkakati wa Marekani kuilazimisha Japan kusalimu amri hatua iliyotimia Agosti 15 1945 na kumaliza vita, pamoja na ukoloni wa Japan barani Asia uliodumu kwa nusu karne.