2,109 waidhinishwa bodi ya Ithibati huku 43 wakwama

KAIMU Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) Wakili Patrick Kipangula, amesema hadi jana Agosti 5, 2025, bodi ilikuwa imepokea maombi zaidi ya 3,200 kwa ajili ya Ithibati na Vitambulisho vya Uandishi wa Habari.

Amesema kati ya maombi hayo tayari maombi 2,109 yameidhinishwa, huku maombi 43 yakikataliwa kutokana na kutokidhi vigezo na 674 yakiwa katika mchakato wa kuthibitishwa.

Amewasihi waandishi wengine ambao bado hawajajisajili kuhakikisha wanafanya hivyo ili waweze kuendelea kutekeleza majukumu yako ya kihabari bila kukinzana na Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii