Bei ya petroli imeshuka huku dizeli ikionekana kupanda

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei kikomo za bidhaa za petroli zitakazotumika hapa nchini kuanzia  Agosti 6 mwaka huu zikionesha kupungua kwa bei ya petroli kwa shilingi 34 kutoka shilingi 2767 hadi shilingi 2743 ya mwezi uliopita ikiwa ni bei ya rejareja kwa mafuta yaliyopokelewa bandari ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara mtawalia. 

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt James Andilile, imeeleza kuwa bei ya petroli katika soko la dunia imepungua kwa 2.3 % huku dizeli ikiongezeka 5.7 % na mafuta ya taa kwa 3.7%.

Vilevile, taarifa hiyo imebainisha kuwa viwango vya kubadilisha fedha,kwa bei za mwezi Agosti, 2025, wastani wa gharama za kubadilidha za kigeni umepungua kwa asilimia 2. 

Kwa upande wa gharama za kuagiza mafuta, kwa Bandari ya Dar es Salaam zimepungua kwa wastani wa 12.3% kwa petroli, 3.11% kwa dizeli na mafuta ya taa zimeongezeka kwa 13.08 % huku bandari ya Tanga kukiwa hakuna mabadiliko. Kwa bandari ya Mtwara, gharama zimeongezeka kwa 6.12% kwa mafuta ya petroli na 60.82%.

EWURA imewakumbusha wafanyabiashara kuuza mafuta kwa bei zilizoidhinishwa na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya yeyote atakayekiuka agizo hilo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii