Hatma ya plastiki yazua mjadala mkali

 MKUTANO wa sita wa wapatanishi wa kimataifa kuhusu mkataba wa marufuku ya plastiki umeanza nchini Uswisi, huku mataifa ya visiwa yakisisitiza umuhimu wa kupitishwa kwa mkataba huo kama sehemu ya mapambano dhidi ya uchafuzi wa mazingira.

Mwakilishi wa Seychelles, Angelique Pouponneau, anayewaongoza wajumbe wa nchi 39 za visiwa, amesema mkutano huo unaofanyika mjini Geneva ni fursa ya mwisho ya kuchukua hatua za kweli kulinda sayari. SOMA: Uzalishaji taka plastiki wasumbua dunia.

Mkurugenzi wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), Inger Andersen, amesema licha ya changamoto zilizopo katika kufikia makubaliano, tatizo la plastiki ni kubwa na linatishia maisha ya viumbe na mazingira.

UNEP imesema kati ya tani milioni 19 hadi 23 za plastiki huingia baharini kila mwaka. Iwapo hatua madhubuti hazitachukuliwa, plastiki inatarajiwa kuchangia asilimia 50 ya uchafu wote baharini ifikapo mwaka 2040.

 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii