Rwanda yapokea wahamiaji 250

 SERIKALI ya Rwanda imeripotiwa kusaini makubaliano na Marekani ya kuwapokea wahamiaji 250 waliotimuliwa nchini humo, katika kile kinachotajwa kuwa sehemu ya mkakati wa Marekani kudhibiti uhamiaji.

Taarifa iliyotolewa na chanzo cha ndani ya serikali ya Rwanda imesema makubaliano hayo yalisainiwa mjini Kigali mwezi Juni, ambapo tayari orodha ya watu kumi wa awali imeshawasilishwa kwa ajili ya usafirishaji.

Msemaji wa Serikali ya Rwanda, Yolande Makolo, amesema nchi hiyo imekubali kushiriki mpango huo kwa kuwa karibu kila familia nchini Rwanda imewahi kupitia mateso ya ukimbizi.

Hatua hiyo imekuja wakati Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump, akiongeza kasi ya kampeni zake kwa kulenga wahamiaji wanaoishi nchini humo bila vibali halali, akipanga kuwahamisha kwa wingi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii