ACT yasisitiza tume ya uchaguzi kuweka wazi vifaa vya uchaguzi

Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Ndugu adoshaibuado ameitaka Tume Huru ya Uchaguzi tumeyauchaguzi_tanzania nchini kuongeza uwazi katika mchakato wa uzalishaji, usafirishaji na uhifadhi wa vifaa vya uchaguzi hasa karatasi za kupigia kura ili kuongeza imani ya wadau wa uchaguzi.

Ndugu Ado Shaibu ametoa rai hiyo wakati akihutubia Mkutano Mkuu katika Jimbo la Kisarawe ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Operesheni Majimaji inayoendesha nchi nzima na Chama hicho kuwahamasisha wanachama wa Chama hicho na wananchi kupiga na kulinda kura zao.

Aidha amesisitiza kuwa wanataka Tume ya Uchaguzi iweke wazi ni kampuni gani imepewa kandarasi ya kuzalisha vifaa vya uchaguzi pamoja na  kujua idadi ya vifaa vingapi vimeagizwa  pia kujua vifaa hivyo vitaingia lini na utaratibu wa kuvihifadhi.

Sambamba na kujua mchakato mzima kwa sababu tatizo la kura feki limewaonesha kuna matatizo pahala kwenye mnyororo mzima wa kura tangu zinapozalishwa hadi zinapopigwa hivyo tume ya Uchaguzi iweke wazi ili kuimarisha imani ya wadau ikiwemo vyama vya siasa na wapiga kura.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii