Mahakama moja Nchini Australia imemkuta Mwanamke aitwae Erin Patterson na hatia ya kuwaua Wakwe zake kwa kuwalisha uyoga wenye sumu katika chakula chao cha mchana miaka miwili iliyopita.
Imeelezwa kuwa siku ya tukio Mwanamke huyo alipokea Wageni ambao walikuwa wanne wakiwemo wawili ambao ni Wazazi wa Mume wake ( Wakwe ) huku hao wengine wawili wakiwa ni Shangazi na Mjomba wa Mume ambapo aliwalisha uyoga huo wenye sumu.
Wiki moja baada ya kujumuika na kula chakula hicho, watatu kati yao walikufa huku Mtu wa nne akinusurika ambapo baada ya vifo hivyo uchunguzi wa Polisi ulianza na kupeleka Erin kushitakiwa kwa kuwapa Wageni wake sumu kwa kukusudia japo mwenyewe alikanusa kufanya makusudi huku akisisitiza kuwa chakula hicho kiliwekewa sumu ya uyoga huo hatari duniani kwa bahati mbaya.
Erin Patterson na Mume wake aitwae Simon walikuwa wakiishi mbalimbali kwa muda mrefu na bado walikuwa kwenye ndoa.