Ajali ya Lori la Mizigo Yatokea Usagara Jijini Mwanza

Lori la mizigo aina ya Fuso lenye namba T290 DDG lililokuwa limebeba shehena ya viazi mbatata limepata ajali jioni ya Machi 12, 2026 majira ya saa 10:00 katika eneo la kiplefti cha Usagara jijini Mwanza.


Kwa mujibu wa taarifa za awali, hakuna kifo kilichoripotiwa katika ajali hiyo. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza lilifika eneo la tukio kwa wakati na linaendelea na taratibu nyingine za uchunguzi.


Madereva wametakiwa kuendelea kuchukua tahadhari wanapokuwa barabarani, hususan katika maeneo ya kona kali, maungio ya barabara na viplefti ili kuepusha ajali.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii