Papa Leo ahuzunishwa na mauaji ya watoto Iran

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Leo XIV (14 ) amesikitishwa na vifo vya raia wengi katika vita vya Iran. Vita vya Israel na Marekani dhidi ya Iran vimeingia siku yake ya 12.

Papa pia ameelezea kuwa karibu na watu wa Lebanon, akisema nchi hiyo inayolengwa kwa mashambulizi ya Israel inapitia wakati mgumu.

Papa Leo amekuwa akitoa wito wa kila mara wa usitishwaji wa mgogoro huo unaoendelea kutanuka, na kuonya kuwa vurugu zinaweza kufikia mahali pa kutoweza kudhibitiwa, amewaomba mahujaji waliofika kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican kuombea amani.

“Tunaendelea kuiombea amani Iran na eneo zima la mashariki ya kati, haswa kwa waathiriwa wote, miongoni mwao watoto. tunawaombea kwamba sala zetu ziwafariji wale wanaoteseka na tunaomba pia matumaini kwa siku zijazo.” amesema.

Vita vya Israel na Marekani dhidi ya Iran vimeingia siku yake ya 12 hii leo, huku Iran ikionya kuwa itaziandama benki na taasisi za fedha zenye mafungamano na Israel na Marekani, katika maeneo ya Ghuba na Mashariki ya Kati kufuatia mashambulizi dhidi ya benki kuu yake mjini Tehran.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii