Raia wa Congo Brazzaville kushiriki uchaguzi mkuu wikendi hii

Raia wa Congo Brazzaville Jumapili ya wiki hii watachagua rais, huku kiongozi wa sasa Denis Sassou Nguesso mwenye umri wa miaka 82 akiwania kwa muhula wa tano ambapo atapambana na wapinzani wengine sita.

N'Guesso,  ambaye ameongoza nchi hiyo kwa miongo minne atakuwa anapeperusha bendera ya chama tawala cha Leba .

Baadhi ya wapinzani wake ni mbunge wa zamani  Mabio Mavoungou Zinga, anayeongoza muungano wa upinzani.

Wengine ni Joseph Kignoumbi Kia Mboungou wa  (La Chaîne),mtaalam wa uchumi  Uphrem Dave Mafoula, Gavet Elengo Melaine Destin wa  Republican Movement, Nganguia Engambé Anguios wa  (PAR) na  Vivien Romain.

Wadadisi wanasema upinzani hauna nafasi kubwa kwenye uchaguzi huu kwa kuwa chama tawala kimekuwa kikidhibiti uongozi wa nchi kwa kutumia vitisho na kufifisha upinzani.

Wapinzani wawili kati ya sita hao wanasemekana kususia kura ya Jumapili.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii