Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limefuta matokeo yote ya Watahiniwa 71 wakiwemo 70 wa Mtihani wa Kidato cha Sita (64 wa Shule na 06 wa Kujitegemea) na mmoja wa Mtihani wa Ualimu Daraja A (GATCE) ambao walibainika kufanya udanganyifu katika Mtihani.
Akiongea Visiwani Zanzibar leo July 07 mwaka huu Katibu Mtendaji wa NECTA, Dr. Said Mohamed amesema “Matokeo hayo yamefutwa kwa mujibu wa Kifungu cha 5 (2) (i) na (j) cha Sheria ya Baraza la Mitihani Sura ya 107 kikisomwa pamoja na Kifungu cha 30(2) (b) cha Kanuni za Mitihani za Mwaka 2016”