Wilaya ya kalambo yapata hati safi miaka 5 mfululizo kwa ukusanyaji wa mapato

Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa kwa mwaka wa fedha 2023/2024 imepata hati safi (inayoridhisha) hatua iliochangiwa na uwepo wa ushirikiano baina ya madiwani na watalaamu pamoja na halmashauri kufanya vizuri katika suala la ukusanyaji mapato kwa kukusanya kiasi cha shilingi 1,935,099,446.00 sawa na asilimia 80.

Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2023/2024 iliyotolewa Aprili, 2025 imeonenyesha kwamba Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo ilikuwa na Hoja za miaka ya nyuma ambazo hazijafungwa 9 na Hoja za Mwaka huu (2023/2024) ni 21 hivyo kufanya kuwa na jumla ya Hoja 30.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mkongoro Nyerere kupitia kikao cha utekelezaji wa hoja za ukaguzi na mapendekezo ya mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2023/2024 kilichofanyika katika Halmashauri ya Kalambo ametumia fursa hiyo kuwaagiza wakurugenzi wa halmashauri za mkoani huo kusimamia kikamilifu ukusanyaji wa Mapato ya Ndani ili kufikia malengo ya halmshauri husika.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii