Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua zoezi la Kampeni ya Chanjo na Utambuzi wa Mifugo Kitaifa, Juni16, 2025 Mjini Bariadi, mkoani Simiyu.
Hayo yamefahamika wakati Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akiongea na Waandishi wa Habari jijini Dodoma leo Juni 11, 2025, ambapo amesema uzinduzi huo wa Kampeni ya chanjo ni sehemu ya juhudi za Serikali katika kuhakikisha inaendelea kuboresha afya ya mifugo hapa nchini ambayo inakadiriwa kuwa na ng’ombe milioni 39.2, mbuzi milioni 28.6, kondoo milioni 9.7, kuku milioni 108.2 na nguruwe milioni 4.1.