ONYO KALI LATOREWA KWA MAKANDARASI

Waziri wa Ujenzi amewaonya vikali makandarasi wanaoshindwa kukamilisha miradi ya ujenzi kwa wakati kwa sababu ya uzembe huku akisema Serikali haitawavumilia wala kuwaongezea muda hata siku moja .

 kauli hiyo imetorewa na Abdallah Ulega mkoani Lindi leo Jumatatu Mei 26, 2025 akiwa katika ziara ya ukaguzi wa miundombinu ya ujenzi wa barabara na madaraja inayotekelezwa katika mikoa ya Kusini kufuatia maelekezo ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya mvua kubwa na kimbunga kuharibu barabara.

Aidha amesisitiza kuwa Serikali imewaamini na kuwapa kazi ya ujenzi wa barabara na madaraja ya kudumu hivyo ni vyema kuharakisha wanakamilisha kazi zeo kwa ubora na kwa wakati na kusema kwamba hawatakubali kuona wananchi wakiteseka tena wakati wa mvua kwa sababu ya uzembe wenu.

Waziri huyo pia amewataka makandarasi kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo kabla ya kuanza kwa mvua za vuli ifikapo Septemba na kusema huu ndio wakati muafaka wa kukamilisha kazi hiyo.







Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii