Maonesho ya madini kuongeza ajira Geita

Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Mohamed Gombati amesema Maonesho ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea mkoani humo kila mwaka yamekuwa yakiongeza ajira na mzunguko wa biashara kwa wananchi, watoa huduma na wafanyabiashara wa mkoa huo.

Gombati amesema pindi maonesho hayo yanapoanza, wafanyabiashara na watoa huduma za usafirishaji, vyakula, malazi, mapambo, ujenzi wa mabanda, huneemeka moja kwa moja na uwepo wake.

"Kipindi hiki cha maonesho ili upate sehemu ya kulala lazima uwe umefanya booking mapema. Hii inaonesha namna wageni walivyojaa Geita kushiriki maonesho ya Teknolojia ya Madini," amesema Gombati.

Amesema hayo Septemba 22, mwaka huu na vyombo vya habari ambapo ameeleza kuwa leo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kufungua rasmi maonesho hayo yaliyoanza Septemba 18 mwaka huu na yanatarajiwa kumalizika Septemba 28 mwaka huu. 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii