CHADEMA waahidi huduma bure kwa Wananchi

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), jimbo la Bukoba Mjini Mkoani Kagera kimezindua rasmi kampeni zake za uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kunadi sera zake huku mawakala wa Chama hicho wakitarajiwa kupewa Semina ya uchaguzi Novemba 25, 2024.

Akizungumza wakati wa kuzindua kampeini za Chama hicho, Mwenyekiti wa CHADEMA Chief Kalumuna huko Kata kashai Mtaa wa mafumbo amewanadi jumla ya wagombea 372 wakiwemo wenyeviti, wajumbe wa makundi mchanganyiko na Wanawake akisema chama hicho kikipewa dhamana kitawahudumia Wananchi bure na kuboresha miundombinu mbalimbali, ikiwemo barabara.

Amesema, Chama hicho kitaendelea kuweka ukweli na uwazi kwa wananchi shughuli zote za kimaendeleo na kusema wagombea wakipewa la lidhaa ya kuwatumikia kila baada ya miezi mitatu watakuwa wanafanya mikutano na kuwaeleza wananchi hali mapato na matumizi.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii