CCM yatoa vipaumbele 9 na washirika 7 walioshiriki katika maandalizi ya Ilani

Ilani mpya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa Uchaguzi Mkuu wa 2025 inalenga kujenga uchumi jumuishi unaowafikia Watanzania wote kuchochea maendeleo ya kisasa, kupunguza umaskini na kuimarisha ustawi wa jamii ambapo ilani hiyo imezinduliwa rasmi leo Mei 30, 2025, ikiwa na vipaumbele vipya vinavyolenga ukuaji wa uchumi, ajira kwa vijana, maendeleo ya teknolojia, elimu, afya, miundombinu na mazingira.

Na hivi ndivyo vipaumbele 9 vya Ilani ya CCM 2025 ikiwemo:

1. Kuchochea Mapinduzi ya Uchumi wa Kisasa
2. Kuongeza Fursa za Ajira kwa Vijana na Kupunguza Umaskini
3. Kuboresha Maisha ya Watu na Ustawi wa Jamii
4. Kuimarisha Miundombinu ya Usafiri na Usafirishaji
5. Kukuza na Kuimarisha Matumizi ya Sayansi na Teknolojia
6. Kudumisha Demokrasia, Utawala Bora na Uwajibikaji
7. Kuendelea Kudumisha Amani, Utulivu na Usalama
8. Kudumisha Utamaduni wa Kitaifa na Kukuza Sanaa na Michezo
9. Kuongeza Kasi ya Maendeleo Vijijini

Ilani hii imeandaliwa kwa makini kwa kuzingatia changamoto za sasa, fursa zilizopo, na matarajio ya Watanzania kwa miaka saba tangu kuanza kwa uchaguzi wa vyama vingi kutoka na maoni  yaliyotolewa na  Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Viongozi wa kisiasa ngazi ya taifa na mikoa, Wawakilishi wa vijana, wanawake na wazee kupitia jumuiya za CCM, Wadau wa sekta binafsi na mashirika ya kiraia, Watafiti na wachumi waliotoa takwimu na tafsiri za kitaalamu za hali ya maendeleo nchini

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii