Enzo Maresca Atajwa Kumrithi Ruben Amorim Manchester United

Jina la Enzo Maresca, kocha raia wa Italia aliyemaliza hivi karibuni kazi yake na klabu ya Chelsea, limo kwenye orodha ya makocha wanaotajwa kuchukua nafasi ya Ruben Amorim.

Uongozi wa Manchester United unaendelea kutathmini majina mbalimbali ya makocha, ambapo Maresca anaonekana kuwa miongoni mwa chaguo linalozingatiwa kwa umakini mkubwa.

Moja ya sababu zinazompa nafasi nzuri Maresca ni uhusiano wake na Omar Berrada, Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Manchester United, ambaye ndiye aliyemleta kocha huyo katika klabu ya Manchester City hapo awali.

Uhusiano huo wa kikazi kati ya Berrada na Maresca unaaminika kuwa unaweza kuwa na mchango mkubwa katika maamuzi ya klabu kuhusu nani atakayekabidhiwa jukumu la kuinoa Manchester United siku zijazo.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii