Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 imeingia hatua ya Robo Fainali ambapo timu nane bora barani Afrika zimejipanga vyema kuwania kufuzu nusu fainali na kuendelea kutafuta ubingwa wa bara.
Robo fainali inatarajiwa kuchezwa tarehe 9 na 10 Januari 2026 ikijumuisha mechi nne za kusisimua zinazotarajiwa kuvutia mashabiki wa soka kutoka pande zote za Afrika.
