Mahakama ya Juu yaidhinisha ushindi wa Mamadi Doumbouya katika uchaguzi wa urais

Mahakama ya Juu nchini Guinea imeeidhinisha siku ya Jumapili jioni, Januari 5, ushindi wa Mamadi Doumbouya katika uchaguzi wa urais wa Desemba 28, kwa asilimia 86.72 ya kura. Jenerali Doumbouya alichaguliwa katika duru ya kwanza kwa muhula wa miaka saba, kufuatia kura iliyosusiwa kwa kiasi kikubwa na vyama vikuu vya upinzani na ambapo viongozi wa upinzani hawakujumuishwa.

Katika hotuba yake ya kwanza kwa taifa baada ya kutangazwa rasmi kwa matokeo, Rais Mteule Mamadi Doumboya alitoa wito kwa Waguinea kuja pamoja ili "kujenga Guinea ya uhuru wa kisiasa na kiuchumi". "Kwa kunipa kura kamili katika duru ya kwanza ya uchaguzi, chaguo lako linanilazimu zaidi. Raia wa Guinea wameonyesha ukomavu, utulivu na utu," alisema.

"Leo, hakuna mshindi wala mshindwa. Kuna Guinea moja tu, iliyoungana na isiyogawanyika",  alisema Rais Mteule Mamadi Doumbouya:

Ushindi wa mgombea huyu binafsi ulitangazwa bila mshangao na Rais wa Mahakama ya Juu, Fodé Bangoura, mbele ya wapinzani ambao hawakujulikana sana na umma kwa ujumla. "Ikizingatiwa kuwa mgombea Mamadi Doumbouya alipata kura nyingi zaidi, alichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Guinea katika duru ya kwanza kwa muhula wa miaka saba," alisema.

Maoni kutoka kwa wagombea na vyama vya siasa

Miongoni mwa wagombea ambao walishindwa, Ibrahima Abé Sylla, wa Kizazi Kipya cha Jamhuri, alimpongeza mshindi na kutoa wito wa umoja wa kitaifa, akiwataka Waguinea "kuungana na kufuata mpango wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa nchi hii".

Hata mpinzani mwingine, Sidibé Ousmane, mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya Rally of Guineans for Prosperity ya Elhadj Bouna Kéita, ambaye anabaini kuwa katika uchaguzi huu ni Guinea iliyoshinda. "Ni hisia ya kuridhika na furaha ninayoieleza mbele ya raia wote wa Guinea. Kwa sababu, zaidi ya yote, leo ni Guinea ambayo inashinda. Ni lazima tukaribishe mienendo ya demokrasia. Ni moyo wa kijamhuri ambao wagombea tisa waliuona na moyo wa ukomavu ambao unapaswa kupongezwa," alibainisha.

Kufuatia kuidhinishwa kwa ushindi wake, Mamadi Doumbouya alitoa wito wa kujengwa kwa "Guinea ya amani na ustawi wa pamoja".

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii