Umoja wa Ulaya kuekeza zaidi eneo la Arctic

Umoja wa Ulaya haujaekeza vya kutosha kwa usalama wa eneo la Arctic na sasa ndio wakati wa kubadilisha hilo na kuekeza zaidi.

Haya yamesemwa na Rais wa Halmshauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula vonder Leyen wakati  akizungumza mjini Brussels, Von der Leyen amesema kuwa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya hivi karibuni itapendekeza kitita kikubwa cha uwekezaji kwa Greenland eneo la Denmark lililo na utawala wa ndani.

Mkuu huyo wa Umoja wa Ulaya ameyasema haya leo kufuatia mkutano wa kilele wa viongozi wa umoja huo ambapo walikuwa wanakutana baada ya mahusiano yao na Marekani kutikiswa na kitisho cha Rais Donald Trump cha kuyawekea mataifa kadhaa ya Ulaya ushuru katika bidhaa zake kwa kukiunga mkono Denmark katika azma yake ya kuzuia kutwaliwa kwa Greenland na Marekani.

Wakati huo huo Rais wa Baraza la Ulaya Antonio Costa amesema kuwa umoja huo utaendelea kujilinda kutokana na ukandamizaji au shinikizo la aina yoyote ile.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii