Tarique Rahman wa BNP aongoza matokeo ya awali Bangladesh

Bangladesh inaingia katika sura mpya ya kisiasa baada ya kufanya uchaguzi wake wa kwanza tangu maandamano makubwa yaliyosababisha kuondolewa madarakani kwa serikali ya Waziri Mkuu wa zamani Sheikh Hasina mwaka 2024.

Katika uchaguzi huo uliofanyika Alhamisi, chama cha Bangladesh Nationalist Party (BNP), kinachoongozwa na Tarique Rahman, kinaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kuunda serikali ijayo, kulingana na matokeo ya awali yaliyotolewa na kituo cha televisheni cha Jamuna TV cha Dhaka.

Ingawa matokeo rasmi yanatarajiwa kutangazwa leo Ijumaa, matokeo ya awali yanaonyesha BNP ikiongoza kwa viti 151, idadi inayotosha kupata wingi wa bunge na hivyo kuunda serikali mpya. Hali hii pia inaibua matarajio kwamba Tarique Rahman, mtoto wa aliyekuwa Waziri Mkuu Khaleda Zia, anaweza kuwa kiongozi ajaye wa taifa hilo.

Uchaguzi huo umetazamwa kama kipimo muhimu cha mustakabali wa demokrasia nchini Bangladesh, hasa baada ya kipindi cha misukosuko ya kisiasa na maandamano ya vijana wa kizazi cha Gen Z yaliyomlazimisha Hasina kukimbilia India.

Tarique Rahman ameahidi kujenga upya taasisi za kidemokrasia, kurejesha utawala wa sheria, na kufufua uchumi ambao umekuwa ukidorora kutokana na misukosuko ya kisiasa. Vyombo vya habari vimeripoti kuwa Rahman alishinda katika majimbo mawili—Dhaka na jimbo lingine la kaskazini anakotoka

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii