Iran yatoa kauli kali, yakataa mazungumzo na United States

Msemaji wa Makao Makuu ya Khatam al-Anbiya ya Iran, Ebrahim Zolfaghari, ametoa kauli kali akilenga United States kuhusu hali ya kisiasa na usalama katika eneo la Middle East.

Kupitia ujumbe wa video ulioripotiwa na vyombo vya habari vya Iran, Zolfaghari amedai kuwa baadhi ya mataifa makubwa yanajaribu kuficha kushindwa kwao kwa kutumia makubaliano, huku akieleza kuwa migogoro ya ndani inaashiria udhaifu wa kisiasa na kimkakati.

Ameonya kuwa taifa hilo halitaendelea kunufaika na uwekezaji wake katika eneo hilo wala bei za zamani za mafuta hadi litakapokubali kuwa utulivu wa Mashariki ya Kati unategemea nguvu ya kijeshi ya Iran na washirika wake.

Aidha, amesisitiza kuwa kwa mtazamo wao, amani na utulivu haviji kupitia mazungumzo pekee bali nguvu ya kijeshi, akihitimisha kwa kueleza kuwa hakuna uwezekano wa kufikiwa makubaliano kati ya pande hizo kwa sasa wala siku zijazo.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii