Iran na Marekani zatofautiana vipengele vya makubaliano

Iran imekanusha kauli ya rais wa Marekani kwamba ilikubali ukaguzi wa nyuklia "usio na kikomo," ikisema haijafikia makubaliano yoyote ya aina hiyo wakati wa mazungumzo ya amani yaliyofanyika nchini Uswisi.

Washington na Tehran zimekuwa zikitoa maelezo yanayokinzana kuhusu vipengele vya makubaliano hayo yaliyosainiwa wiki iliyopita, hasa kuhusu masuala ya kifedha kwa Iran, udhibiti wa Mlango Bahari wa Hormuz, na vita vya Israel dhidi ya Hezbollah nchini Lebanon.

Rais Donald Trump anakabiliwa na ukosoaji kuhusu vita hivyo na Iran huku akikosa uungwaji mkono wa ndani. Kura za maoni zinaonyesha kuwa umaarufu wake unapungua huku Baraza la Seneti linalodhibitiwa na chama chake cha Republican limepitisha hapo jana muswada wa kusitisha vita hivyo, ikiwa ni ishara ya wazi ya mpasuko ndani ya chama chake.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii