Zaidi ya wapiga kura milioni 3.2 wamejiandikisha kushiriki katika uchaguzi wa rais nchini Republic of the Congo ambapo Rais Denis Sassou Nguesso mwenye umri wa miaka 82 anatetea nafasi yake.
Hata hivyo, uchaguzi huo unatajwa kukabiliwa na upinzani dhaifu baada ya baadhi ya viongozi wa upinzani kuwekwa gerezani na wengine kuwa uhamishoni, huku vyama kadhaa vya upinzani vikisusia mchakato huo kwa madai kuwa haukuwa wa kuaminika.