Donald Trump Aongeza Muda wa Kusitisha Mashambulizi kwa Iran

Rais wa United States, Donald Trump, amesema ameongeza muda wa kusitisha mashambulizi dhidi ya viwanda vya nishati vya Iran kutoka siku chache hadi kufikia Aprili 6.

Aidha ameeleza kuwa Iran ilikuwa imeomba kusitishwa kwa mashambulizi kwa siku saba, lakini Marekani ikaamua kuongeza muda huo hadi siku kumi, akidai kuwa hatua hiyo imepokelewa vyema na upande wa Tehran.

Hata hivyo kupitia mtandao wa Truth Social, Trump alithibitisha kuongeza muda huo, huku akisema mazungumzo kati ya Marekani na Iran yanaendelea vizuri.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii