Nicolás Maduro apinga kesi ya Marekani akidai kunyimwa haki

Rais wa zamani wa Venezuela Nicolas Maduro anatarajiwa kufika tena mahakamani Marekani akijaribu kushawishi jaji afute kesi inayomkabili ya ugaidi wa dawa za kulevya.

Anadai serikali ya Marekani inamzuia kupata fedha za kujitetea kisheria, hivyo kuvunja haki yake ya msingi.

Awali, kesi hiyo ilipangwa ili kumpa muda yeye na mke wake Cilia Flores kupitia ushahidi na kujiandaa kwa hatua za kisheria.

Hata hivyo, wakili wake amesema anaweza kujiondoa kwenye kesi hiyo ikiwa serikali ya Venezuela haitaruhusiwa kulipa gharama zake, kutokana na vikwazo vya Marekani vinavyoizuia nchi hiyo kufanya malipo hayo.

Serikali ya Marekani imesema hairuhusu matumizi ya fedha za serikali iliyowekewa vikwazo kulipia mawakili, lakini bado wanaruhusu Maduro kutumia fedha zake binafsi.

Aidha Maduro anapinga hatua hiyo akisema inamnyima haki ya kujitetea. Lakini wataalamu wa sheria wanaona ana nafasi ndogo ya kushinda hoja hiyo.

Hata hivyo yeye na mke wake wamekanusha mashtaka yanayowahusisha na biashara ya dawa za kulevya na silaha kwa zaidi ya miaka 25, na kwa sasa wanashikiliwa gerezani New York.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii