Mwenyekiti wa CHADEMA, Mhe. Tundu Lissu, amewasili katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, akiwa amebeba vifurushi vilivyojaa makabrasha tayari kwa kuendelea na usikilizwaji wa kesi inayomkabili.
Lissu alionekana akiwa na nyaraka hizo akijiandaa kukabiliana na ushahidi wa mashahidi wa upande wa Jamhuri, katika hatua inayoashiria utayari wake wa kujibu hoja zinazowasilishwa mahakamani.
Kesi hiyo inaendelea kusikilizwa mbele ya jopo la majaji watatu, huku mashahidi wa upande wa mashtaka wakiendelea kutoa ushahidi wao.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime