Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetaka kufutwa kwa uchaguzi uliofanyika Oktoba 29 na kuvunjwa kwa Tumehuru ya Uchaguzi nchini (INEC) kwa madai kuwa haukuwa huru wala wa haki.
Akitoa msimamo wa chama hicho leo, baada ya kikao cha kamati kuu ya chama hicho, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho bara John Heche amesema wanaunga mkono makundi yote ya kijamii yaliyoukosoa uchaguzi huo na waangalizi wa uchaguzi waliotoa maoni yao kuhusu uchaguzi huo.
"Ripoti za waangalizi wa uchaguzi ikiwamo kutoka SADC, AU na EAC zinaonesha wazi ukosefu wa uwanja sawia na uhalali wa uchaguzi mambo yote yaliyoainishwa katika ripoti zao yanaimarisha msimamo wa CHADEMA kuendelea kudai mabadiliko ya kikatiba, kisheria na kitaasisi ili hatimaye Tanzania iweze kuendesha shughuli zilizo huru za uchaguzi mbele ya macho ya Watanzania na jumuiya za kimataifa" amesema John Heche.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime