Chadema yapeleka kampeni ya No reforms no election wilayani Simanjiro

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) John Heche amepeleka kampeni ya 'No reforms, No election' kwa wafugaji wa jamii ya Kimaasai akitumia uwekezaji kwenye viwanda vya kusindika nyama na mazao mengine ya mifugo kama kete ya kuwashawishi wafugaji kukiunga mkono chama hicho.

Akihutubia katika mkutano wa hadhara eneo la Mirerani Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara Mei 29 mwaka huu Heche amewahidi kuwa Chadema ikiingia madarakani itajenga siyo tu viwanda vya kusindika mazao ya mifugo bali pia itachimba mabwawa na kujenga miundombinu muhimu ili kuhakikisha wafugaji wanapata uhakika wa maji na malisho kwa mifugo yao.

Aidha amesema kwa utajiri wa mifugo, uoto wa asili na vipindi vya mvua, Wilaya ya Simanjiro inafaa kuwa wilaya ya ufugaji kuwezesha siyo tu wafugaji kufaidika kiuchumi, bali pia Taifa kuingiza fedha za kigeni kwa kuuza mazao ya mifugo yaliyoongezwa thamani, ikiwemo nyama nje ya nchi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii