Aliyekuwa kiongozi wa Chama cha upinzani Misri amechwa huru sasa.

Kiongozi wa upinzani nchini Misri, Ahmed al-Tantawi, ameachiliwa huru baada ya kufungwa jela kwa mwaka mmoja kutokana na makosa ya ukiukwaji wa sheria za uchaguzi kutokana na taarifa iliyotolewa na Wakili wake Khaled Ali alithibitisha habari hiyo kupitia mtandao wa X.

Al-Tantawi alikuwa mpinzani mkuu wa rais wa sasa Abdel Fattah al-Sissi, katika uchaguzi wa mwaka 2023 na aliondolewa katika kinyang'anyiro hicho baada ya kushindwa kupata uungwaji mkono wa kutosha jambo lilopelekea  kuituhumu serikali na wafuasi wa Al-Sissi kwa kuwasumbua waungaji mkono wake.

Mnamo Februari 2024 alihukumiwa pamoja na wasaidizi wake 22 akiwemo msimamizi wa kampeni kwa makosa ya kusambaza fomu zisizoruhusiwa za kuidhinisha kugombea kwake.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii