Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Joseph Kabila ameonekana kwa mara ya kwanza tangu kuondolewa kinga ya kutoshtakiwa na seneti huku akionyesha nia ya kujitokeza tena kisiasa Kabila ambaye alikutana na viongozi wa kidini katika mji wa Goma eneo linalodhibitiwa na waasi wa M23 akielezea dhamira yake ya kusaidia kurejesha amani katika mkoa huo.
Askofu Mkuu Joel Amurani wa Jukwaa la Madhehebu ya Dini amesema Kabila aliwaalika ili kuonyesha msimamo wake wa kutaka utulivu ambopo tumemweleza kwamba bado ana nafasi ya kubeba jukumu la mpatanishi ambao aliutumikia Kwa miaka 18 taifa hili na bado ana uwezo wa kuisaidia nchi kurejea kwenye umoja.
Kabila ambaye aliongoza Kongo kuanzia mwaka 2001 hadi 2019 anakabiliwa na tuhuma nzito za kushiriki katika uasi, uhalifu wa kivita, na uhalifu dhidi ya ubinadamu, hasa kwa kuunga mkono waasi wa M23 wanaodaiwa kupata msaada kutoka serikali ya Rwanda kutokana na tuhuma zilizoibuliwa na Waziri wa Sheria wa Kongo, Constant Mutamba.
Katika hatua ya bunge kuondoa kinga ya seneta wa maisha imeibua mjadala kuhusu mustakabali wa Kabila kisiasa na kisheria Ingawa serikali haijatoa taarifa rasmi kuhusu Kabila kushtakiwa kwa nafasi yake katika siasa za Kongo Wakosoaji wanaamini kurejea kwake Goma ni hatua ya kimkakati kujijenga upya kisiasa katika eneo lililoathiriwa na janga la kibinadamu na ukosefu wa utawala wa sheria.
Hata hivyo Kabila alikuwa uhamishoni kwa hiari tangu mwaka 2023 lakini alirejea nchini mwezi Aprili na kuelekea mashariki mwa Kongo, wakati ambapo serikali ya Rais Félix Tshisekedi ikiendelea kukabiliana na changamoto za kiusalama.
Wakati huo baadhi ya wachambuzi wakishuhudia kurejea kwake kama juhudi za upatanishi kwa wengine wanao amini kuwa wenda ikawa mbinu ya kujinusuru na mikono ya sheria hali hiyo imefanya waasi wa M23 kuendelea kudhibiti miji mikuu mashariki mwa nchi huku mamilioni ya raia wakiendelea kuyahama makazi yao.
Ili kupata taarifa zaidi endelea kutufuatilia kupitia website yetu ya www.jembenijembe.com kupitia Instagram ,Facebook, tikok,x zamani twitter pamoja na YouTube