Rekodi za mrithi wa Trent Alexander Arnold ni balaa

KATIKA raundi ya 26 ya Ligi Kuu England, Liverpool waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Manchester City kwenye dimba la Etihad, kwa mabao ya Mohamed Salah na Dominik Szoboszlai.

Hata hivyo, takwimu zimeonesha jambo la kushangaza: beki wa kulia wa Liverpool, Trent Alexander-Arnold, alipitwa na wachezaji kwa 'dribbles' mara 12 katika mechi hiyo pekee — idadi kubwa mno kwa mchezaji mmoja katika mchezo mmoja.

Kwa kulinganisha, Jeremie Frimpong, ambaye anatarajiwa kujiunga na Liverpool alipitwa kwa dribbles mara 13 tu katika msimu mzima wa Bundesliga 2024–25. Hii inaonesha tofauti ya ulinzi kati ya wawili hao, na kile ambacho Frimpong anaweza kuleta katika safu ya ulinzi ya Liverpool.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii