Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Ndg. Gerson Msigwa amesema
Michezo ni ajira uchumi na inatangaza Tanzania na sasa mchezo wa ngumi umekua miongoni mwa michezo inayokuwa kimataifa.
Alisema hayo Oktoba 10 mwaka huu katika viwanja vya Posta Kijitonyama Dar es Salaam kwenye mashindano na ngumi (Knock Out ya Mama) ambapo alisema, Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anaendelea kuunga mkono mashindano hayo kwa Milioni kumi na Milioni ishirini pamoja na ujenzi wa miundombinu ya michezo ya ndani (Arts and Sport Arena) na viwanja vya mpira wa Miguu mikoa mbalimbali.