Uteuzi huu unamweka Karia katika historia kama Mtanzania wa kwanza kushika nafasi ya juu ndani ya uongozi wa FIFA, hatua inayodhihirisha hadhi na heshima inayoongezeka kwa soka la Tanzania katika ngazi ya kimataifa.
Aidha, Karia ni miongoni mwa Marais watano pekee wa mashirikisho ya soka barani Afrika walioteuliwa na FIFA kushika nafasi mbalimbali katika kamati zake kuu, jambo linaloonesha imani kubwa ya shirikisho hilo kwa viongozi wa Afrika.