Kiungo Liverpool atwaa tuzo, awabwaga Cole Palmer na wenzake

KIUNGO wa Liverpool Ryan Gravenberch ametwaa tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi wa Msimu wa Ligi Kuu England (EPL) 2024-25.

Mholanzi huyo amepewa heshima hiyo kutokana na kiwango bora alichoonesha msimu huu, akicheza katika nafasi mpya ya kiungo wa kati wa ulinzi chini ya kocha mpya Arne Slot.

Tangu asajiliwe kutoka Bayern Munich mwaka 2023, Gravenberch amekuwa chuma cha kati katika kikosi cha Liverpool kilichotwaa ubingwa wa EPL mapema mwezi Aprili, huku yeye akianza mechi zote 34 hadi timu ilipohakikisha ubingwa wake.

Ameshinda tuzo hiyo baada ya kuwashinda nyota wengine waliotajwa kwenye orodha fupi, wakiwemo Liam Delap, Anthony Elanga, Dean Huijsen, Cole Palmer, Joao Pedro, Morgan Rogers na William Saliba.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii